Let us know! Organising a viewing party?

About / Kuhusu

TEDxIlala is an independently organized TEDx event and will be happening for the first time in 2015. Our aim is to bring people together and share ideas in the heart of the city of Dar es Salaam. The theme for our event will be Yes, In My Lifetime.

TEDxIlala ni tukio la TEDx lililoandaliwa na watu binafsi na litafanyika kwa mara ya kwanza hapa mwaka huu 2015. Lengo letu ni kuwakusanya watu hapa mjini Dar es Salaam kuweza kujadili mada tofauti na kubadilishana mawazo. Mandhari ya tukio ni Yes, In My Lifetime.

About / Kuhusu TED & TEDx

In the spirit of ideas worth spreading, TED has created a program called TEDx. TEDx is a program of local, self-organized events that bring people together to share a TED-like experience. Our event is called TEDxIlala, where x = independently organized TED event. At our TEDxIlala event, TEDTalks video and live speakers will combine to spark deep discussion and connection in a small group. The TED Conference provides general guidance for the TEDx program, but individual TEDx events, including ours, are self-organized.

Katika hali ya kusambaza maarifa yenye thamani na manufaa, TED imeunda mpango uitwao TEDx. TEDx ni mpango wa hapahapa au wakienyeji unaopanga wenyewe tukio au mkusanyiko wa watu waje kuchangiana mawazo kwenye mpango wa TED. Tukio au kongamano letu ndio linaitwa TEDxIlala, ambapo “x” ni tukio la TED lililopangwa nasiwenyewe. Kwenye tukio au kongamano letu la TEDxIlala, TEDTalks itawaleta wazungumzaji wenyewe au kupitia video ili waweze kushiriki kwa kuchangia mada zenye kina paweze kuwepo majadiliano ya hali ya juu kwenye kikundi kidogo. Kongamano kuu la TED litatoa muongozo wa jumla kwa ajili ya program za TEDx, lakini pia matukio mengine madogo madogo ya TEDx pamoja na hili letu yatapangwa yenyewe na wahusika au walengwa.

About / Kuhusu TED

TED is a nonprofit organization devoted to Ideas Worth Spreading. Started as a four-day conference in California 30 years ago, TED has grown to support its mission with multiple initiatives. The two annual TED Conferences invite the world’s leading thinkers and doers to speak for 18 minutes or less. Many of these talks are then made available, free, at TED.com. TED speakers have included Bill Gates, Jane Goodall, Elizabeth Gilbert, Sir Richard Branson, Nandan Nilekani, Philippe Starck, Ngozi Okonjo-Iweala, Sal Khan and Daniel Kahneman.

TED ni shirika lisilonufaika lenye lengo la kusambaza maarifa mazuri yenye thamani kwenye jamii.TED ilianzishwa baada ya kongamano la siku nne lililofanyika huko California miaka thelathini iliyopita. TED imekua nakuweza kupigania na kutetea ujumbe na lengo lake kwa kutumia mbinu na nyenzo tofauti. Makongamano ya TED mawili makubwa ya mwaka hua yanaalika viongozi wenye maarifa ya hali ya juu na watendaji tofauti tofauti kuja kuzungumza kwa dakika zisizozidi 18 kila mmoja. Halafu haya mazungumzo na risala zina wekwa kwenye tovuti ya TED.com ili watu wanufaikenazo bila kulipia. Mifano ya waliowahi kushiriki kwenye matukio haya na kutoa risala za kuwaongoza watu ni pamoja na: Bill Gates, Jane Goodall, Elizabeth Gilbert, Sir Richard Branson, Nandan Nilekani, Philippe Starck, Ngozi Okonjo-Iweala, Sal Khan na Daniel Kahneman.

The annual TED Conference takes place each spring in Vancouver, British Columbia, along with the TEDActive simulcast event in nearby Whistler. The annual TEDGlobal conference will be held this October in Rio de Janeiro, Brazil. TED’s media initiatives include TED.com, where new TED Talks are posted daily; the Open Translation Project, which provides subtitles and interactive transcripts as well as translations from volunteers worldwide; the educational initiative TED-Ed. TED has established the annual TED Prize, where exceptional individuals with a wish to change the world get help translating their wishes into action; TEDx, which supports individuals or groups in hosting local, self- organized TED-style events around the world, and the TED Fellows program, helping world-changing innovators from around the globe to amplify the impact of their remarkable projects and activities.

Mkutano mkubwa wa mwaka wa TED hufanyika kila kipindi cha kuchipua, yaani baada ya kipindi cha baridi, huko Vancouver nchini Canada, pamoja na tukio la TEDActive linalofanyika mji wa karibu hapo Whistler. Mkutano mwingine mkubwa wa mwaka wa TEDGlobal utafanyika Oktoba hii huko Rio de Janeiro, nchini Brazil. Mbinu za usambazaji taarifa kuhusu TED kupitia vyombo vya habari na mitandao zinatumika kwa mfano kupitia tovuti ya TED.com ambapo risala mpya zinatangaziwa siku hadi siku. Pia kuna zoezi la kutafsiri (Open Translation Project) linaloshirikisha watu wanaojitolea muda wao duniani kote kutafsiri kazi za TED na kuna Nyanja nyingine ya TED inayohusu elimu inayoitwa TED-Ed. TED nayo imeanzisha tuzo la kila mwaka, TED Prize, wanalopewa watu binafsi wenye malengo makubwa ya kuboresha maisha duniani ili waweze kutekeleza hizo ndoto zao zikaja kuwa kweli. TEDx inajukumu lingine kubwa lakuwasaidia watu binafsi au hata makundi kuandaa matukio na makongamano yanayojitegemea sehemu nyingi duniani. Kuna program nyingine nayo inayoitwa TED Fellows Program inayo walenga wabunifu duniani kote na kuwawezesha kukuza wigo na matokeo ya shughuli zao na ubunifu wao.

Follow TED on Twitter at http://twitter.com/TEDTalks, or on Facebook at http://www.facebook.com/TED.

Kuifuata TED kwenye Twitter: http://twitter.com/TEDTalks au kwenye Facebook: http://www.facebook.com/TED

x = independently organized event